• HABARI MPYA

    Friday, November 26, 2021

    RUVU SHOOTING YAICHAPA KAGERA 2-1


    WENYEJI, Ruvu Shooting wameibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya Kagera Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Mabatini, Mlandizi mkoani Pwani.
    Mabao ya Ruvu yamefungwa na Zuberi Dabi dakika ya 30 na Rashid Juma dakika ya 84, wakati la Kagera Sugar limefungwa na Ally Nassor dakika ya 84.
    Kwa matokeo hayo, Ruvu inafikisha pointi tisa na kusogea nafasi ya sita, wakati Kagera Sugar inabaki na pointi zake nane katika nafasi ya saba baada ya wote kucheza mechi saba.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: RUVU SHOOTING YAICHAPA KAGERA 2-1 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top