• HABARI MPYA

    Thursday, June 18, 2009

    MISS TZ WA KWANZA...


    Mwaka 1960 ndipo Mashindano ya urembo nchini yalipoanza na hayatakuwa na muonekano wa kimataifa kwa sababu yalifanyika kwenye maeneo machache.Kwani kumbukumbu zilizopo zinaonyesha kwamba mrembo wa kwanza kunyakua taji hilo la Miss Tanzania, si mwingine bali alikuwa Theresa Shayo.Kutokana na maadali na utamaduni ya mtanzania serikali ililazimika kuyapiga marufuku mashindano hayo ilipofika tu mwaka 1967, kabla ya Rais wa awamu ya pili Alhaj Ali Hassan Mwinyi kuyaruhusu kuendelea kutokana na utandawazi kuanza kushika kasi ya ajabu.Tangu kipindi hicho nchi yetu ya tanzania iliweza kufanikiwa kutoa warembo kadhaa walioshiriki mashindano ya kumtafuta mrembo wa dunia, wakiwemo Emil Adolf, Nancy Sumary, Saida Kessy, Basila Mwanukuzi, Hoyce Temu, Jacqueline Ntuyabaliwe na wengineo. Mshindi huyo wa kwanza kushiriki mashindano hayo ya urembo ya Miss Tanzania Theresa Shayo, alifariki dunia huko Augburg Munich Ujerumani na kuzikwa uko uko alikokuwa akiishi miaka yote hiyo.Mwaka 1967 ndipo hayati Theresa alitwaa taji hilo kwenye shindano lilofanyika hoteli ya Kilimanjaro, alifariki dunia january 26 mwaka 2007 na maradhi ya kansa ya tumbo huku akiwa na umri wa miaka 61.Theresa hakubahatika kupata mtoto na alikuwa akiishi mjini Augsburg ambako aliolewa na mjerumani aitwaye Chrstian Rieger ambaye waliachana na hadi anakufa alikuwa akiishi na boy friend aitwaye Tonny.Kabla ya hapo Theresa alikuwa akiishi peke yake mtaa wa Schmiedberg namba 9 katikati ya mji wa Augsburg na alimwachia nyumba hiyo mtanzania aitwaye Othman Lukindo.Kwani alikuwa ni mtu mwenye huruma sana pamoja na kwamba alijiengemeza zaidi kwa ndugu zetu wa Kenye, alikuwa na upendo na kila mmoja uko alikokuwa akiishi alimpenda.Mashindano haya yamekuwa yakitia fora na kujizolea umaarufu mkubwa ndani ya jamii ya watanzania, hasa baada ya kuwa chini ya uratibu wa Hashim Lundega, ambaye alianza kuyaendesha tangu mwaka 1994. Kwani kupitia Lundega, kampuni mbalimbali zimekuwa zikijitokeza kudhamini mashindano hayo na kutoa zawadi zikiwemo za magari ya kisasa kwa washindi, hali iliyoyafanya yawe na ushindani mkali. Ukuaji wa Mashindano haya ulikuwa ni wa kasi kubwa kwani watu wengi kama ilivyo kwa mchezo wa soka ama muziki, hasa baada ya muziki wa kitanzania kuingiliwa na vionjo vya kutoka nchi jirani ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo). Mkoa wa Mbeya nao haupo nyuma katika mashindano hayo. Umekuwa unapita katika hatua hizo kwa kupata warembo mbalimbali walioibuka washindi kuanzia ngazi ya mkoa, kanda hadi kufikia hatua ya kushiriki shindano la 'Miss Tanzania'.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MISS TZ WA KWANZA... Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top