KLABU za Liverpool na Barcelona zitakuwa na mazungumzo mazito juu ya kuuziana Luis Suarez wiki hii baada ya klabu ya Hispania kutoa ofa ya wazi ya Pauni Milioni 72.
Bado dau hilo ni dogo kulingana na like wanalotaka Liverpool, Pauni Milioni 80, lakini linaonyesha mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 27 yuko njiania kuondoka.
Kikao cha jana mjini London kilikuwa kilichozalisha rasmi mpango wa biashara hiyo kwa panda zote mbili.
Mtendaji Mkuu wa Liverpool, Ian Ayre alikutana na mawakala wa nguvu wa Barcelona, Raul Sanllehi, Toni Rossich na Jordi Mestre.
Pamoja na hao hakuna kilichokamilishwa ila kuna matarajio maafikiano yatafikiwa na Suarez anaweza kuhamia Barcelona.
Liverpool imeendeleza nia yake ya kumtaka Alexis Sanchez na anaweza akajumuishwa katika mango huo huku Liverpool tayari ikiwa imemthaminisha kwa Pauni Milioni 30.
Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Chile bado hajapewa taarifa coyote kuhusu kuhamia Anfield na uhamisho wa Suarez hauwezi kukamilishwa hadi nyota huyo mwenye umri wa miaka 25 aamue kujiunga na Liverpool, au Arsenal, ama klabu nyingine Ulaya au kubaki Nou Camp.



.png)
0 comments:
Post a Comment