• HABARI MPYA

    Tuesday, July 01, 2014

    HUMUD NA WENGINE WANNE WAPATA TIMU NJE

    Na Boniface Wambura, DAR ES SALAAM
    WACHEZAJI watano wameombewa Hati ya Uhamisho ya Kimataifa (ITC) ili waweze kucheza mpira wa miguu nchini na nje ya Tanzania.
    Abdulhalim Humoud kutoka Simba, Crispine Odulla (Coastal Union) na Haji Ugando (Mbagala Market FC) wameombewa ITC na Shirikisho la Mpira wa Miguu la Kenya (FKF) ili wakacheze nchini humo katika klabu za Sofapaka, Bandari FC na Nakuru All Stars.
    Abdulhalim Humud anakwenda Sofapaka

    Vilevile TFF imemuombea ITC mchezaji Ismaila Diarra kutoka nchini Mali ili aweze kujiunga na timu ya Azam FC. TFF inafanyia kazi maombi hayo, na mara taratibu zote zitakapokamilika itatoa ITC hizo kwa wachezaji wanaokwenda nje ya Tanzania.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: HUMUD NA WENGINE WANNE WAPATA TIMU NJE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top