KOCHA wa Uruguay, Oscar Tabarez amesema Luis Suarez anaendelea kuimarika baada ya kufanyiwa upasuaji, lakini amekubali kwamba hatacheza kwa ubora ule aliokuwa nao katika Ligi Kuu ya England.
Mshambuliaji huyo wa Liverpool amekuwa akisumbuliwa na maumivu ya goti tangu kabla ya kuanza kwa Kombe la Dunia, lakini baada ya kipigo cha kushitua kutoka kwa Costa Rica anatarajiwa kurudi uwanjani dhidi ya Three Lions kesho.
Tabarez amegoma kuthibitisha iwapo atamuanzisha au la mkali huyo wa mabao.
Anaendelea vizuri: Goti la Suarez lililofanyiwa upasuaji siku chache kabla ya Kombe la Dunia



.png)
0 comments:
Post a Comment