AIBU gani hii! Hispania imevuliwa ubingwa wa dunia usiku huu baada ya kuchapwa mabao 2-0 na Chile katika mchezo wa Kundi B Uwanja wa Maracana, Rio de Jeneiro, Brazil.
Maana yake, Hispania watacheza mechi ya kukamilisha ratiba dhidi ya Australia kisha kurejea nyumbani mapema, wakiiacha michuano bado mibichi kabisa.
Mabao yaliyoizamisha Hispania leo yamefungwa na
Eduardo Vargas dakika ya 19 na Charles Aranguiz dakika ya 43 - hivyo ukijumlisha na kipigo cha 5-1 walichopewa na Uholanzi maana yake hawana maisha tena katika Fainali za Brazi 2014.
Uholanzi na Chile zote zina pointi sita kila moja, wakati Australia na Hispania hazina pointi. Kwa Chile ushindi wa leo ni sawa na kulipa kisasa cha kufungwa 2-1 nchini Afrika Kusini mwaka 2010 katika mchezo wa mwisho wa kundi kwenye michuano hiyo.
Mwanzo mzuri: Eduardo Vargas akishangilia baada ya kuifungia Chile bao la kwanza dhidi ya Hispania
Kocha Vicente Del Bosque atajutia uamuzi wa kuendelea kumpanga kipa Iker Casillas, kwani kwa mara nyingine leo amefungwa mabao ya ‘kibwege’.
Kikosi cha Hispania kilikuwa; Casillas, Azpilicueta, Martinez, Ramos, Alba, Busquets, Alonso/Koke dk46, Silva, Iniesta, Pedro/Cazorla dk77 na Costa/Torres dk64.
Chile; Bravo, Medel, Silva, Jara, Isla, Aranguiz/Gutierrez dk64, Diaz, Mena, Vidal/Carmona dk88, Vargas/Valdivia dk85 na Sanchez.
Amekwisha: Vargas akimtungua kiulaini kipa aliyechuja Iker Casillas



.png)
0 comments:
Post a Comment