• HABARI MPYA

    Wednesday, May 01, 2013

    YANGA KAMA MAN UNITED, YATOA SARE BAADA YA KUTWAA UBINGWA

    Mfungaji wa bao la Yanga leo, Jerry Tegete
    Na Prince Akbar
    MABINGWA wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Yanga SC jioni hii wameshindwa kuwapa zawadi ya ubingwa mashabiki wao, baada ya kulazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Coastal Union ya Tanga kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
    Kwa sare hiyo, Yanga imefikisha pointi 57 baada ya kucheza mechi 25, wakati Coastal iliyocheza mechi sawa na hizo, imetimiza pointi 35 na inabaki nafasi ya sita.
    Katika mchezo huo, uliochezeshwa na refa Simon Mberwa kutoka Pwani, aliyesaidiwa na Said Mnonga na Charles Chambea wote wa Mtwara, hadi mapumziko timu hizo zilikuwa tayari zimekwishafungana bao 1-1.
    Yanga waliotwaa taji la Ligi Kuu wiki iliyopita, ndio waliokuwa wa kwanza kupata bao dakika ya tatu, mfungaji Jerry Tegete. 
    Tegete ambaye mara ya mwisho alifunga Februari 13 mabao mawili katika ushindi wa 4-0 dhidi ya African Lyon kwenye Uwanaj huo huo, leo alifungia bao hilo la kwanza baada ya kupokea pasi ya kiungo Nurdin Bakari dakika ya tatu tu ya mchezo huo.
    Bao hilo, halikudumu sana, kwani dakika ya 16, Abdi Banda aliisawazishia Coastal Union na kufanya dakika 45 za kipindi cha pili pia kiishe matokeo yakiwa 1-1.
    Katika mchezo huo, kikosi cha Yanga SC kilikuwa; Said Mohamed, Mbuyu Twite, Oscar Joshua, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Kevin Yondan, Nurdin Bakari, Nizar Khalfan, Frank Domayo, Said Bahanuzi/Joseph Banda dk67, Jerry Tegete na Abdallah Mnguli/Haruna Niyonzima dk67.
    Coastal Union; Shaaban Kado, Hamad Khamis, Othman Tamim, Philip Mugenzi, Yussuf Chuma, Abdi Banda, Joseph Mahundi, Razack Khalfan, Pius Kisambale/Mohamed Soud dk66, Suleiman Kassim ‘Selembe’ na Danny Lyanga.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: YANGA KAMA MAN UNITED, YATOA SARE BAADA YA KUTWAA UBINGWA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top