![]() |
| Damayo |
KLABU za Simba, Yanga na Azam tangu juzi zinapigana vikumbo
kuwania saini ya kiungo mkabaji wa JKT Ruvu, chipukizi Frank Damayo na hadi
sasa hakuna timu ambayo imefanikiwa kuinasa.
BIN ZUBEIRY imezungumza na Damayo mwenyewe amesema ni kweli
timu zote hizo na nyingine mbili, Mtibwa Sugar na Coastal Union zinamfuatilia ila
hadi hadi saa 5:00 usiku alikuwa hajasaini timu yoyote.
Damayo alisema timu inayomtaka kwanza lazima izungumze na
klabu yake na maelekezo atakayopewa na mwajiri wake ndiyo atakayoyafuata.
Damayo amekuwa lulu ghafa, baada ya kucheza soka ya kuvutia
katika mchezo wa Kundi C kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Kombe la Dunai
Jumapili kati ya Tanzania na Gambia.
Katika mechi hiyo ambayo Taifa Stars iliwatungua Nge wa Gambia
2-1, Damayo alicheza kwa uelewano mkubwa na Kelvin Yondan na kiungo wa juu,
Mwinyi Kazimoto, wote wachezaji wa Simba.
Yondan amesaini Yanga, ingawa na klabu yake, Simba SC ambayo
pia anachezea Mwinyi Kazimoto aliyetokea JKT Ruvu pia inadai ina mkataba naye
na sasa hatima yake itategemea makubaliano baina ya klabu hizo mbili zinazomgombea.



.png)
0 comments:
Post a Comment