Tetesi za J'tano magazeti Ulaya
LIVERPOOL YAPATA KIFAA CHA MAANA
MWANASOKA wa kimataifa wa Iceland, Gylfi Sigurdsson mwenye umri wa miaka 22 atajiunga na Liverpool kwa dau la pauni Milioni 7, ingawa awali alikuwa tayari kujiunga na klabu ya Swansea.
KLABU ya ipo kwenye nafasi nzuri ya kumsajili mshambuliaji wa Montpellier, Olivier Giroud, mwenye umri wa miaka 25, kwa mujibu wa kocha wa klabu yake, Rene Girard.
BEKI wa Lille, Mathieu Debuchy, mwenye umri wa miaka 26, ambaye amekuwa akihusishwa na mpango wa kuhamia Newcastle,amesema ataamua mustakabali wake baada ya Euro 2012.
KOCHA mpya wa West Brom, Steve Clarke amemtaja beki wa NEC Nijmegen, mwenye thamani ya pauni Milioni 2, Bram Nuytinck, mwenye umri wa miaka 22, kama mchezaji anayemtaka zaidi kikosini mwake.
KLABU ya West Ham inaongoza mbio za kuwania saini ya mshambuliaji wa Sochaux, Modibo Maiga. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 24 wa Mali, ilibaki kidogo tu atue Newcastle Januari, lakini dili hiyo ilikufa kutokana na matatizo yake ya goti.
KLABU ya West Ham, 'The Hammers' pia inamtaka kwa udi na uvumba winga mwenye thamani ya pauni Milioni 4 wa Wolves na timu ya taifa ya England, Matt Jarvis.
REDKNAPP NJE SPURS
KOCHA wa Tottenham, Harry Redknapp bado anaweza kuondoka White Hart Lane wakati wowote, licha ya kukanusha tetesi kwamba amejiuzulu.
MWENYEKITI wa klabu ya Tottenham, Daniel Levy anafikiria aidha kumfukuza kocha wa sasa wa klabu hiyo, Harry Redknapp baada ya kukosa nafasi ya kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao.
KLABU ya Chelsea itamtaja Roberto Di Matteo kamaq kocha wao rasmi mpya, baada ya kukwama kwa mazungumzo yao na kocha aliyebwaga manyanga Barcelona, Pep Guardiola.
KLABU ya Swansea City ina matumaini ya kumtaja mrithi wa aliyekuwa kocha wao, Brendan Rodgers aliyetimkia Liverpool, kutoka orodha waliyonayo inayoongozwa na Ian Holloway na Michael Laudrup.
BOSI wa Shirikisho la Soka Ukraine, Grygoriy Surkis amewakoromea England kwa kushikia bango suala la ubaguzi na kusema kwamba wajadili suala la kuenguliwa kwa utata kwenye kikosi hicho kwa beki Rio Ferdinand.
SHEVCHENKO APATA AJALI
JEZI za mpya za mechi za nyumbani za Manchester City ambazo bado ni siri, zimepelekwa Australia kwa ajili ya mauzo- wiki kadhaa kabla ya kuzinduliwa kwake rasmi Uingereza.
SAA kadhaa baada ya kufanya 'mavituuz' katika Euro 2012, mshambuliaji wa Ukraine, Andriy Shevchenko alihusika kwenye ajali ya gari katikati ya jiji la Kiev.



.png)
0 comments:
Post a Comment