• HABARI MPYA

    Monday, June 01, 2015

    DOKTA AJITOKEZA KUWANIA UENYEKITI COASTAL UNION

    Na Mwandishi Wetu, TANGA
    KUELEKEA Uchaguzi Mkuu wa Klabu ya Coastal Union tayari maandalizi yameanza kukamilika kwa asilimia kubwa ambapo jumla ya wagombea kumi na tano wamejitokeza kuchukua fomu kuwania nafasi mbalimbali za
    uongozi.
    Akizungumza leo mjini hapa, Ofisa Habari wa Coastal Union,Oscar Assenga amesema katika uchaguzi mkuu nafasi ambazo wagombea wamejitokeza ni Mwenyekiti
    ambapo nafasi hiyo amejitokeza Dk. Ahmed Twaha akiwa hapa mpinzani.
    Nafasi ya makamu Mwenyekiti wamejitokeza wagombea wawili ambao ni Salim Amiri na Hussein Abdull Ally ambao watachuana ili kuweza kupatikana mshindi ambayo atachukua nafasi hiyo.
    Kikosi cha Coastal Union inayoshiriki Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara

    Aidha, amesema kuwa katika nafasi ya Kamati ya utendaji wamejitokeza wagombea kumi na mbili ambao watachuana na kubaki wajumbe watano watakaounda kamati ya utendaji.
    Amewataja waliojitokeza kuwania nafasi hiyo ni Albert Clement Peter, Omari Mwambasha, Waziri Mohamed, Mohamed Ally 'Dondo', Mohamed Maulid Rajab, Abubakar Ahmed Machai, Aggrey Ally Mbapu, Hassani Omari Bwana.
    Wengine ambao wamejitokeza kuwania nafasi hiyo kuwa ni Abdallah Zuberi Ally 'Unenge', Hassan Ramadhani Muhsin, Albert Clement Peter, Hussein Ally Mwinyi Hamis na Salim Abasi Perembo.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: DOKTA AJITOKEZA KUWANIA UENYEKITI COASTAL UNION Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top