IMEWEKWA JUNI 4, 2013 SAA 2:00 ASUBUHI
BAADA ya kukamilisha uhamisho wake kutua Barcelona, Neymar ambaye anaungana na Lionel Messi kuunda safu mpya kali ya ushambuliaji, ameweka wazi malengo yake.
Mbrazil huyo alisafiri moja kwa moja kwenda Hispania baada ya Brazil kutoa sare ya 2-2 nyumbani na England mjini Rio de Janeiro Jumapili, na katika mahojiano aliyofanyiwa kwenye Uwanja wa Nou Camp alisema: "Nipo kumsaidia na kumsaidia Messi kuendelea kuwa mchezaji bora duniani,".
Neymar alipokewa kifalme katika Uwanja wa Ndege wa Barcelona - kabla ya kupelekwa kwenye ofisi za klabu hiyo kwa ajili ya kupigwa picha akiwa na jezi ya Blaugrana kisha kwenda kufanyiwa vipimo vya afya.
Neymar alitambulishwa kuwa mchezaji mpya wa Barcelona Nou Camp jana
Mbrazil huyo amesaini Mkataba wa miaka mitano Catalan
Neymar akionyesha uwezo wake wa kuchezea mpira mbele ya umati wa Nou Camp
Neymar anaungana na 'mchawi' huyu Lionel Messi kuunda safu kali ya ushambuliaji Barcelona
Rais wa Barcelona, Sandro Rosell akimkaribisha Neymar Nou Camp
Neymar akipungia mkono mashabiki Nou Camp
Neymar akisalimiana na mashabiki watoto wa Barca Uwabnja wa Nou Camp
Neymar akifanyiwa vipimo vya afya


.png)