• HABARI MPYA

    Tuesday, April 10, 2012

    NADAL, NOVAK KUPAMBANA BERNABEU

    Nadal
    WACHEZAJI wawili bora wa tenisi duniani, namba moja na namba mbili, Novak Djokovic na Rafa Nadal, watajaribu kuweka rekodi katika kwa mahudhurio kwenye mechi ya mchezo huo, wakati watakapomenyana kwenye Uwanja wa Real Madrid, Bernabeu mwezi Julai, klabu hiyo imesema leo.
    "Gumzo kubwa kwenye ni kuweka rekodi kwenye mchezo wa tenisi katika Uwanja huu wa kuchukua mashabiki 80,000," ilisema taarifa hiyo ya klabu bingwa Ulaya mara tisa.
    Mechi hiyo ya hisani inayotarajiwa kuchezwa Julai 14, imeandaliwa na mfuko wa hisani wa Real Madrid kwa pamoja na mfuko wa Rafa Nadal.
    Mspanyola Nadal ni shabiki anayefahamika sana wa Real wakati Mserbia, amekuwa mgeni rasmi katika vifaa vya ya klabu hiyo, na mara moja alivaa jezi ya Real wakati akitembea kabla ya mechi ya tenisi katika Madrid Masters.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: NADAL, NOVAK KUPAMBANA BERNABEU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top