SIKWENDA kwenye onyesho lao kubwa la kutambulisha bendi yao pale Dar Live Mbagala, lakini kwa mujibu wa simulizi za waliohudhuria, kuna makosa mengi ya kiufundi yalijitokeza wakati wakiwa jukwaani.
Hata walipotumbuiza katika tamasha la Fiesta ndani ya viwanja vya Leaders, hawakufanya kile kilichotarajiwa, walipiga show ya kawaida sana.
Lakini walipogiga na Twanga Pepeta kwenye ukumbi wa New White Hosue Kimara, walitia fora, kila walichofanya kiliwatia wazimu mashabiki, wakavutia kwa kila jambo kwa aina ya mashabiki waliohudhuria onyesho hilo.
Jumapili ya wiki iliyopita wakafanya tena onyesho na Twanga Pepeta Leaders Club, wakatesa, wakafurahisha na kuwapeleka msobemsobe mashabiki, naskia hata walipofanya onyesho la shangwe za Eid El Hajj pale Escape One, onyesho lililohudhuriwa na umati mkubwa wa watu, walifanya vizuri.
Lakini katika onyesho lao ndani ya tamasha la Siku ya Msanii pale Mlimani City Oktoba 26, walikuwa chini ya kiwango, kulikuwa na dosari nyingi za kiufundi, dosari nyingi za kisaikolojia, dosari nyingi za matumizi ya jukwaa.
Naizungumzia YAMOTO BAND, bendi inayoundwa na waimbaji wanne wa kiume - waimbaji chipukizi lakini wenye vipaji vya hali juu, Dogo Aslay, Beka, Enock Bella na Maromboso.
Yamoto ni bendi inayotoka katika taasisi ya muziki ya Mkubwa na Wanawe inayoongozwa na mtu mwenye kujua ipasavyo fitna za muziki – SAID FELLA.
Ni bendi yenye nyimbo kali zikiwemo “Yamoto”, “Bora Kijijini, “Nitajuta (Nibemende)” na “Niseme Nisiseme” ambazo zimeshika chati kila kituo cha radio, kila mtaa, kila uchochoro, si wakubwa, si wadogo ili mradi kila mtu anapagawa na Yamoto Band.
Nataka nizungumzie walichokifanya kwenye tamasha la Siku ya Msanii – tamasha la kipekee kwa madhumuni ya kipekee ndani ya ukumbi wa kipekee wenye hadhi ya kipekee na kuhudhuriwa na watu wengi wenye hadhi ya kipekee akiwemo Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt Mohammed Gharib Bilal.
Kwa hali hiyo basi wengi tulitarajia pia kupata burudani ya kipekee kutoka kwa wasanii wa kipekee waliochaguliwa kutumbuiza kwenye tamasha hilo, lakini haikuwa hivyo kwa wadogo zangu wa Yamoto Band.
Kuna wakati Yamoto walionyesha kuwa wana uwezo wa kujipanga mstari mmoja na kushambulia jukwaa kwa pamoja, lakini katika hali ya kushangaza, hayo waliyafanya kwa bahati mbaya na badala yake wakatumia muda mwingi kutawanyika huku na kule, mwingine yuko kulia, mwingine kushoto, mwingine anatazamana na wapiga vyombo, mwingine yuko mbele ya jukwaa, hali iliyopunguza msimsiko wa show yao.
Kuna wakati wakawa wanaimba kama vile wako kwenye sanaa ya ngonjera - huyu anatoka upande mmoja wa jukwaa na kumfuata mwenzake mbio na kwenda kudakia kipande cha uimbaji kinachofutia, Yamoto wakasahau kuwa walipewa heshima kubwa ya kufanya show ya kuhitimisha tamasha lile, wakitanguliwa na wasanii wengi wenye majina makubwa akiwemo Diamond.
Wadago zangu Yamoto mna nyimbo nyingi nzuri sana, sana tu, wala hamkuwa na haja ya kuimba nyimbo za kina Msagasumu pale, mambo ya naipenda Simba mshabiki wa damu, naipenda Yanga mshabiki wa damu hayakuwa mahala pake pale, pengine hamkujua lakini niwajuze kuwa watu wengi walianza kutoka ukumbini dakika 15 tu baada ya nyinyi kuwa jukwaani. Nilijiuliza sana, ule ujanja wa matumizi ya jukwaa uliokuwa unaonyeshwa kwenye show za TMK Wanaume Family iliyokuwa chini ya uongozi wa Fella, kwanini haujawaambukiza wadogo zao hawa wa Yamoto? Hata sipati jibu.
Hata mlivyoingia jukwaani na kuanza kutoa salam kupitia vipaza sauti haikuwa poa, unamsalimia nani? Habari za jioni, sijui usiku mlipaswa kuwaachia ma –mc na watoa hotuba, nyinyi kazi yenu ilikuwa ni burudani tu, kumbukeni namna Diaomond alivyoingia jukwaani.
Hakika mna vipaji, mkituliza akili mtafika mbali, wengi wetu tunawatazama kama warithi wa wanamuziki dansi wa sasa. Mmepata bahati kubwa sana nyimbo zenu zinapigwa kwenye vipindi vya bongo fleva, vipindi vya muziki mchanganyiko na hata vipindi vya dansi, Mungu awape nini tena? Chonde chonde supu msiitie nazi, Sikinde walituambia supu yake ni ndimu na pili pili, ukitia nazi ujue umeharibu.

.png)
0 comments:
Post a Comment