• HABARI MPYA

    Monday, November 03, 2014

    MSUVA AANGUKA BAFUNI, ATENGUA KIUNO…JAVU NAYE GOTI, YANGA SC WAREJEA LEO DAR

    Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
    WINGA Simoni Msuva wiki iliyopita alianguka bafuni na kutonesha kiuno chake kilichomuweka nje ya Uwanja kwa wiki mbili, hali iliyomsababisha aendelee kukosekana katika timu yake, Yanga SC.
    Hata hivyo, kulingana na maendeleo yake, kuna uwezekano Msuva akarudi uwanjani wikiendi hii, Yanga SC ikicheza na Mgambo JKT Jumamosi Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
    Msuva amekuwa mpishi mzuri wa mabao katika klabu ya Yanga SC siku za karibuni, na zaidi inaaminika ndiye anayeweza kumlisha mpira ya kufunga mshambuliaji Mbrazil wa timu hiyo, Genilson Santana Santos ‘Jaja’.
    Msuva anaweza kurudi uwanjani Jumamosi

    Kukosekana kwake, kumemfanya Jaja afunge bao moja tu katika mechi tatu zilizopita, ambalo alifunga Yanga SC ikishinda 3-0 dhidi ya Stand United mjini Shinyanga. 
    Aidha, mshambuliaji Hussein Javu naye anasumbuliwa na maumivu ya goti- na anatarajiwa kwenda kufanyiwa vipimo wiki hii katika hospitali ya Rufaa ya Muhimbili.
    Yanga SC inatarajiwa kurejea Dar es Salaam leo ikitokea Bukoba, ambako Jumamosi ilifungwa 1-0 katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara na wenyeji Kagera Sugar.  
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MSUVA AANGUKA BAFUNI, ATENGUA KIUNO…JAVU NAYE GOTI, YANGA SC WAREJEA LEO DAR Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top