• HABARI MPYA

    Sunday, May 10, 2026

    PAMBA JIJI YAAMBULIA SULUHU KWA DODOMA JIJI 0-0 KIRUMBA


    WENYEJI, Pamba Jiji FC wamelazimishwa sare ya bila mabao na Dodoma Jiji FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza.
    Kwa matokeo hayo, Pamba Jiji FC inafikisha pointi 30, ingawa inabaki nafasi ya saba ikiizidi pointi moja Dodoma Jiji FC inayofuatia nafasi ya nane baada ya timu zote kucheza mechi 22 katika Ligi Kuu inayoshirikisha timu 16.  
    Ikumbukwe mwisho wa msimu timu mbili zitashuka Daraja na mbili zitakazomaliza nafasi ya 14 na 13 zitamenyana baina yao kwa mechi mbili za nyumbani na ugenini na mshindi wa jumla atasalia Ligi Kuu.
    Timu itakayofungwa itakwenda kumenyana na timu kutoka Ligi ya Championship katika mechi nyingine mbili za mchujo nyumbani na ugenini na mshindi wa jumla ndiye atacheza Ligi Kuu msimu ujao.  

     

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: PAMBA JIJI YAAMBULIA SULUHU KWA DODOMA JIJI 0-0 KIRUMBA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top