• HABARI MPYA

    Sunday, May 10, 2026

    FOUNTAIN GATE YAWALAZA KMC FC MABAO 3-2 PALE PALE MWENGE


    TIMU ya Fountain Gate imeibuka na ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya wenyeji, KMC FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa KMC Complex, Mwenge, Dar es Salaam.
    Mabao ya Fountain Gate yamefungwa na mshambuliaji mzawa, Sadick Said Ramadhani ‘Immobile’ dakika ya 28 na Wanigeria, mshambuliaji McDonald Obas dakika ya 61 na kiungo Henry David dakika ya 86, wakati ya KMC yamefungwa na winga Edson Erick Mwijage dakika ya 30 na mshambuliaji Rashid Mohamed Chambo dakika ya 68.
    Kwa ushindi huo, Fountain Gate inafikisha pointi 25 na kusogea nafasi ya 10 kutoka ya 12, wakati KMC inaendelea kushika mkia kwenye ligi ya timu 16 ikibaki na pointi zake tisa baada ya kila timu kucheza mechi 22. 
    Ikumbukwe mwisho wa msimu timu mbili zitashuka Daraja na mbili zitakazomaliza nafasi ya 14 na 13 zitamenyana baina yao kwa mechi mbili za nyumbani na ugenini na mshindi wa jumla atasalia Ligi Kuu.
    Timu itakayofungwa itakwenda kumenyana na timu kutoka Ligi ya Championship katika mechi nyingine mbili za mchujo nyumbani na ugenini na mshindi wa jumla ndiye atacheza Ligi Kuu msimu ujao.  
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: FOUNTAIN GATE YAWALAZA KMC FC MABAO 3-2 PALE PALE MWENGE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top