“WATER”
“WATER”
“SAFINA”
“NGANO
“UNGA
“UNGA
HABARI ZA NYUMBANI

NYOTA ANAYECHEZA SOKA YA KULIPWA AZERBAIJAN AITWA TAIFA STARS

KOCHA Mkuu wa timu ya soka ya taifa Tanzania, Hemed Suleiman ‘Morocco’ amemjumuisha kiungo Alphonce Mabula Msanga (21) anayechezea klabu ya Shamakhi FK ya Ligi Kuu ya Azerbaijani kwenye kikosi cha wachezaji 28 kitakachokwenda Afrika Kusini kucheza michuano ya Kombe la Mataifa ya Kusini mwa Afrika (COSAFA).
Akizungumza na Waandishi wa Habari mapema leo Jijini Dar es Salaam, Morocco amesema kikosi hicho cha Taifa Stars kitaingia kambini Jumatatu na Jumanne kitasafiri kwenda Afrika Kusini kwa ajili ya michuano hiyo inayotarajiwa kuanza Juni 4 Uwanja wa Free State Toyota mjini Bloemfontein nchini Afrika Kusini.
Kabla ya kwenda kwenye michuano ya COSAFA, Taifa Stars itacheza mchezo mmoja wa kirafiki na wenyeji, Bafana Bafana Juni 6 kuanzia Saa 2:30 usiku Uwanja wa Peter Mokaba Jijini Polokwane, Pietersburg.
Mabula aliibukia akademi ya Alliance ya Mwanza kabla ya kwenda Serbia ambako alichezea klabu za FK Spartak Subotica mwaka 2022, RFK Novi Sad 2023, akarudi Spartak Subotica 2024 hadi Januari mwaka huu alipojiunga na Shamakhi FK.


Kwenye Kombe la COSAFA Tanzania imeorodheshwa dakika za mwisho baada ya Morocco kujitoa na imepangwa Kundi C pamoja na Ewatini na Madagascar, wakati Kundi A wapo wenyeji Afrika Kusini, Mauritius, Msumbiji na Zimbabwe na Kundi B linazikutanisha Angola, Lesotho, Malawi na Namibia.
Taifa Stars itacheza mechi yake ya kwanza ya COSAFA Juni 7 dhidi ya Madagascar kabla ya kumalizia na Eswatini Juni 11 kuagalia mustakabali wake wa kwenda Nusu Fanali ambazo zitafuatia Juni 13 na Fainali ni Juni 13 sambamba na mechi ya kusaka mshindi wa tatu.
Mara ya mwisho Tanzania ilishiriki michuano ya COSAFA mwaka 2017 Jijini Rusternburg nchini Afrika Kusini na kutolewa katika hatua ya Nusu Fainali ikifungwa mabao 4-2 na Zambia Julai 5, mabao ya Taifa Stars yakifngwa na Erasto Nyoni dakika ya 16 na Simon Msuva dakika ya 85, huku ya Chipolopolo yakifungwa na Brian Mwila dakika ya 44, Justin Shonga mawili dakika ya 45+2′ na 68 na Jackson Chirwa kwa Penalti dakika ya 56.
Taifa Stars ilianza vyema kwa kuongoza Kundi A mbele ya Angola, Mauritius na Malawi ikivuna ponti tano na kuizidi tu wastani wa mabao Angola, huku Mauritiusn na Malawi kila moja ikiambulia pointi mbili.
Taifa Stars ambayo mechi zake za Kundi A iliifunga Malawi 2-0 na kutoa sare ya 0-0 na Angola na 1-1 na Mauritius – kwenye Robo Fanali iliwatoa wenyeji, Bafana Bafana bao pekee la mshambuliaji Elias Maguri dakika ya 18.

KIKOSI KAMILI TAIFA STARS:
Makipa; Yakoub Suleiman (JKT Tanzania), Ally Salim (Simba SC), Hussein Masaranga (Singida Black Stars) na Anthony Remy (Azam FC U20.
Mabeki:), Miraj Abdallah (Coastal Union), Shomari Kapombe (Simba SC), Mohamed Hussein (Simba SC), Lusajo Mwaikenda (Azam FC), Pascal Msindo (Azam FC), Vedastus Masinde (TMA Stars), Wilson Nangu (JKT Tanzania), Abdulrazak Hamza (Simba SC), Ibrahim Ame (Mashujaa FC), Abdulrahim Bausi (JKT Tanzania), Ibrahim Abdullah (Yanga SC) na Dickson Job (Yanga SC).
Viungo: Alphonce Mabula (Shamakhi FK, Azebairjan), Ahmed Bakari Pipino (KMC FC), Idrisa Stambuli (Mashujaa FC), Yusuph Kagoma (Simba SC), Shekhan Khamis (Yanga SC), Feisal Salum (Azam FC), Kibu Dennis (Simba SC), Iddi Suleiman (Azam FC), Suleiman Mwalimu (Wydad FC, Moriocco) na Simon Msuva (Al-Talaba, Iraq).
Washambuliaji: Valentino Mashaka (Simba SC) na Mishano Daudi (Ken Gold).

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button