“MARINE”    
“SAFINA”
“NGANO
“UNGA
“UNGA
“WATER”
HABARI ZA KIMATAIFAHABARI ZA ULAYA

UFARANSA YAICHAPA UJERUMANI 2-0 NA KUSHINDA NAFASI YA TATU LIGI YA ULAYA

MSHAMBULIAJI Kylian Mbappe amefunga bao lake la 50 katika timu ya taifa ya Ufaransa ikiibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya wenyeji, Ujerumani katika mchezo wa kuwania nafasi ya tatu Ligi ya Mataifa ya Ulaya leo Uwanja wa MHPArena Jijini Stuttgart.
Nahodha huyo wa Ufaransa alimalizia vyema pasi ya mchezaji mwenzake wa Real Madrid, Aurelien Tchouameni kuipatia timu yake bao la kwanza dakika ya 45.
Mbappe akamsetia Michael Olise kufunga bao la pili dakika sita kabla ya filimbi ya mwisho akitumia makosa ya Robin Koch na bila ya uchoyo akatoa pasi kwa mfungaji aliyetumbukiza mpira nyavuni lango likiwa wazi.
Ujerumani ilipata nafasi pia lakini zote penalti waliyopewa na bao walilofunga vilibatilishwa baada ya marudio ya Picha za Video (VAR).
Kwanza Karim Adeyemi alipewa penalti baada ya yeye mwenyewe kuangushwa na kipa wa Ufaransa, Mike Maignan, lakini mshambuliaji huyo wa Ujerumani akaishia kuonyeshwa kadi ya njano baada ya VAR kuonyesha alijiangusha.
Na tena Deniz Undav akafunga bao ambalo nalo lilikataliwa baada ya VAR kuonyesha Niclas Fullkrug alimchezea faulo Adrien Rabiot katika ujenzi wa shambulizi lililosababisha bao hilo.
Huo unakuwa mchezo wa tatu kwa Kocha Julian Nagelsmann kutoshinda ikiwemo na Nusu Fainali ambayo walifungwa Ureno 2-1.
Baada ya ushindi huo, Kocha wa Les Bleus, Didier Deschamps alimsifu Mike Maignan kwa kazi nzuri katika safu ya ulinzi.

Kyllian Mbappe akiwa na Tuzo ya Mchezaji Bora wa mechi hiyo Ufaransa ikiifunga Ujerumani 2-0

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button