“MARINE”    
“SAFINA”
“NGANO
“UNGA
“UNGA
“WATER”
HABARI ZA AFRIKAHABARI ZA ASIA

RAIS WYDAD AFICHUA DILI LA KUMSAJILI RONALDO LILIVYOFELI

RAIS wa klabu ya Wydad Athletic ya Casablanca nchini Morocco, Hicham Ait-Menna amesema kwamba walijaribu bila mafanikio kumsajili Mwanasoka Bora wa zamani wa Dunia, Cristiano Ronaldo ili wamtumie katika Klabu Bingwa ya Dunia ya FIFA.
Ronaldo aliyebakiza wiki chache kumaliza mkataba wake Al Nassr alihusishwa kuhamia timu nyingine kwa ajili ya michuano hiyo ya FIFA na Morocco ilitajwa kwa pamoja na Brazil.
Hata hivyo, mambo yaligeuka ghafla baada ya Ronaldo kuiwezesha Ureno kutwaa taji la Ligi ya Mataifa ya Ulaya, UEFA Nations League akasema hana mpango wa kucheza Klabu Bingwa ya Dunia ya FIFA.
Wydad Casablanca ilikuwa moja kati ya klabu zilizotaka kumpa mkataba wa mud mfupi Ronaldo na Ait-Menna amethibitisha kujaribu kumsajili mkongwe huyo wa umri wa miaka 40.
“Cristiano Ronaldo asingekuja kwa sababu ya fedha, kwa sababu hakuhitaji. Sijui namna hizi yeye si zilisambaa, lakini ni ukweli kwamba niliwasiliana na mmoja wa marafiki wa mawakala wake miezi mitatu na nusu au minne iliyopita na akamuambia; Asingependa kucheza Klabu Bingwa ya Dunia,’ amesema.
Vizuri, Sifikirii hiyo,”.
“Hakukuwa na majadiliano haswa kwa ajili ya mchezaji hiyo. Tungependa kuwa naye, lakini kifedha tusingeweza kutoa malipo yanayolingana na thamani yake. Vinginevyo, alionyesha dhamira..
Nilirejea kwake mara mbili au tatu,”.
Ronaldo alisema alipokea mapendekezo mengi ya kucheza Klabu Bingwa ya Dunia na ilitarajiwa amgejiunga na Al Hilal ya Saudi Arabia pia kwa mkopo kwenye michuano hiyo ya FIFA.
Kwa sasa Ronaldo yupo kwenye mazungumzo a Al Nassr over kwa ajili ya kuongeza mnataka baada ya hivi karibuni kuweka banana anapenda kubaki.

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button