“MARINE”    
“SAFINA”
“NGANO
“UNGA
“UNGA
“WATER”
HABARI ZA AFRIKA

MAMELODI SUNDOWNS YAANZA VYEMA KOMBE LA DUNIA LA FIFA

TIMU ya Mamelodi Sundowns jana imeanza vyema michuano ya Kombe la Klabu Bingwa ya Dunia ya FIFA baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Ulsan HD ya Korea Kusini bao la mshambuliaji Iqraam Rayners dakika ya 36 katika mchezo wa Kundi F Uwanja wa Inter&Co Stadium, Orlando, Marekani.
Na baada ya Borussia Dortmund ya Ujerumani kulazimishwa sare ya 0-0 na Fluminense ya Brazil katika mchezo wa mwingine wa hilo usiku wa jana Uwanja MetLife, East Rutherford – sasa Mamelodi inaanzia kileleni mwa Kundi F.
Nayo Inter Milan ya Italia ikalazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Monterrey ya Mexico katika mchezo wa Kundi E Uwanja wa
Rose Bowl, Pasadena.
Mkongwe beki Sergio Ramos García (39) alianza kuifungia Monterrey dakika ya 25, kabla ya mshambuliaji Muargentina, Lautaro Javier Martínez kuisawazishia Inter Milan dakika ya 42.
Mchezo uliotangulia wa kundi hilo, River Plate ya Argentina iliitandika Urawa Red Diamonds ya Japan mabao 3-1 Uwanja wa Lumen Field, Seattle.
Mabao ya River Plate yalifungwa na wazawa yote – mshambuliaji Facundo Colidio dakika ya 12, kiungo Sebastian Driussi dakika ya 48 na winga Maximiliano Meza dakika ya 73, huku bao pekee la Urawa Red Diamonds likifungwa na winga mzawa pia, Yusuke Matsuo kwa penalty dakika ya 58.

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button