“SAFINA”
“NGANO
“UNGA
“UNGA
“WATER”
HABARI ZA AFRIKA

AL AHLY MABINGWA LIGI KUU MISRI MARA YA 45

TIMU ya Al Ahly imefanikiwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Misri kwa mara ya 45 baada ya ushindi wa mabao 6-0dhidi ya Pharco FC Uwanja wa Cairo International Jijini Cairo.
Ilikuwa siku nzuri kwa mshambuliaji wa Kimataifa wa Palestina, Wessam Abou Ali aliyefunga mabao manne katika mchezoo huo dakika za 10, 33, 61 na 66, huku mabao mengine yakifungw ana Hussein El Shahat dakika ya 75 na Emam Ashour dakiika ya 90’+3.
Ushindi huo umeifanya Al Ahly kumaliza msimu ikiwa na pointi 58, mbili zaidi ya Pyramids FC, ambao waliilaza Ceramica Cleopatra mabao 5-1 lakini wakaambulia patupu.
Mashetani Wekundu walianza msimu huu chini ya Marcel Koller, lakini ni kocha wa muda Emad El-Nahhas ambaye aliwaongoza hadi hatua ya mwisho, na kupata ushindi mara sita mfululizo na kutumia Pyramids kuteleza ili kutwaa ubingwa.
Al Ahly walimaliza kampeni wakiwa na rekodi bora za ushambuliaji na ulinzi, mabao 52 na kufungwa 18 pekee.
Miamba hao wa Cairo sasa wanatarajia kuhamishia cheche zao katika michuano ya Klabu Bingwa ya Dunia ya inayotarajiwa kuanza Juni 14 hadi Julai 13 nchini Marekani ikishirikisha timu 32 kutoka Mabara sita – nne kutoka Afrika, Al Ahly ya Misri, Espérance ya Tunisia, Mamelodi Sundown ya Afrika Kusini na Wydad Athletcs ya Morocco.
Al Ahly imepangwa Kundi A pamoja na Palmeiras ya Brazil, FC Porto ya Ureno na Inter Miami CF ya Marekani, wakati Wydad imepangwa Kundi G pamoja na Manchester City ya England, Al Ain ya Falme za Kiarabu (UAE) na Juventus ya Italia.

Mamelodi Sundowns wapo Kundi F pamoja na Fluminense ya Brazil, Borussia Dortmund ya Ujerumani na Ulsan HD ya Korea Kusini na Espérance Kundi D pamoja na Flamengo ya Brazil, Chelsea ya England na mshindi wa mechi ya mchujo kati ya Los Angeles FC ya Marekani na América ya Mexico.

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button