“MARINE”    
“SAFINA”
“NGANO
“UNGA
“UNGA
“WATER”
HABARI ZA AFRIKA

KAIZER CHIEFS YAMUACHA MSHAMBULIAJI RANGA CHIVAVIRO

KLABU ya Kaizer Chiefs imeachana na mshambuliaji Ranga Piniel Chivaviro (32) baada ya misimu miwili ya kuwa naye kufuatia kumaliza mkataba wake.
Taarifa ya Kaizer Chiefs jioni ya leo imesema kwamba haitaongeza mkataba na mchezaji huyo mzaliwa wa Limpopo kwa mama Muafrika Kusini na baba Mziimbabwe baada ya mkataba wake kumalizika mwishoni mwa mwezi.
“Kaizer Chiefs haitaongeza mkatab a wa mshambuliaji Ranga Chivaviro utakapomalizika mwishoni mwa mwezi. Tunamshukuru Ranga kwa mchango wake chanya kwenyd timu na tunamtakia kila la heri katika mafanikio yake yajayo,” imesema taarifa ya Kaizer.
Kaizer inaachana na Chivaviro kutokana na mchezaji huyo kutofanya vizuri msimu wake wa mwisho wa mkataba wake akifunga mabao matano tu katika mechi 22 za mashindano yote, jambo liliamsha hasira za mashabiki dhidi yake waliokuwa wakimzomea.
Kwa msimu wa pili mfululizo, Amakhosi wamemaliza nje ya Nane Bora kwenye Ligi Kuu ya Afrika Kusini – ingawa tu wamefanikiwa kutwaa Kombe la Nedbank ambalo limemaliza ukame wa mataji wa klabu hiyo kwa muda mrefu wa muongo.
Ranga Chivaviro aliibukia Witbank Spurs ya Mpumalanga mwaka 2013, kabla ya kuhamia Cape Town All Stars ya Johanesburg mwaka 2016, ambako alicheza kwa miezi kadhaa akahamia Ubuntu Cape Town ya Cape Town hadi mwaka 2018 akaenda Baroka ya Ga-Mphahlele karibu na Polokwane, Limpopo.
Mwaka 2019 alikwenda kujiunga na TS Sporting ya Zwelisha, karibu na Mbombela, Mpumalanga kwa mkopo hadi mwaka 2021 akaenda Trepça ya Kosovo hadi mwaka 2021 akarejea Afrika Kusini kujunga na Venda FA ya Venda hadi mwaka 2022 aliposajiliwa na Marumo Gallants alikocheza hadi mwaka 2023 alipojiunga na Kaizer Chiefs.

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button