“WATER”
“WATER”
“SAFINA”
“NGANO
“UNGA
“UNGA
HABARI ZA KIMATAIFAHABARI ZA ULAYA

XABI ALONSO NDIYE KOCHA MPYA WA REAL MADRID

RAIS wa Real Madrid, Florentino Pérez amemtambulisha Xabi Alonso kuwa kocha mpya wa klabu hiyo kwa mkataba wa misimu mitatu ijayo, kuanzia 1 Juni 2025, hadi 30 Juni 2028 akirithi mikoba ya Mtaliano, Carlo Ancelotti aliyeondoka baada ya msimu mbaya uliomalizika.
President Florentino Pérez alimkaribisha Xabi kwenye chumba cha mikutano cha Real Madrid City, ambako alisaini mkataba na kukabidhiwa jezi yenye jina lake na vitu vingine kabla ya kupelejkwa Uwanjani.
Xabi Alonso ni gwiji wa Real Madrid na mmoja wa wachezaji wakubwa katika historia ya soka duniani akiwa amewahi kuichezea mechi 236 kuanzia mwaka 2009 hadi 2014 na kushinda mataji sita kipindi hicho, ambayo ni taji la 10 la Ligi ya Mabingwa Ulaya Jijini Lisbon nchini Ueno, Super Super moja ya Ulaya, La Liga moja, mawili ya Kombe la Mfalme na Super Cup moja ya Hispania.
Xabi Alonso pia anajivunia mafanikio yake katika timu ya taifa ya Hispania, ambayo aliichezea jumla ya mechi 113 na kushinda nayo mataji matatu, ambayo ni Kombe la Dunia mwaka 2010 na Kombe la Mataifa ya Ulaya, Euro mara mbili mwaka 2008 na 2012.
Xabi Alonso alianza taaluma yake ya ukocha katika akademi ya Real Madrid, akifundisha timu za Vijana za U-12 na kuiwezesha kubeba taji la Torneo de Campeones 2018-2019.
Mwamba Sasa anarejea Real Madrid kama mmoja wa makocha wakubwa duniani baada ya kuweka historia katika klabu ya Bayer Leverkusen ya Ujerumani, ambayo aliiwezesha kushinda matajia ya Bundesliga, Kombe la Ujerumani na Super Cup ya Ujerumani akimaliza msimu wa 2023-2024 bila kupoteza mechi.

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button