“MARINE”    
“SAFINA”
“NGANO
“UNGA
“UNGA
“WATER”
HABARI ZA NYUMBANI

AZAM FC NA FOUNTAIN GATE ZAINGIA FAINALI LIGI YA VIJANA U20

TIMU za Azam FC na Fountain Gate zitakutana katika Fainali ya Ligi ya Vijana chini ya umri wa miaka 20 kesho kuanzia Saa 1:00 usiku Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam baada ya kuzitoa Kagera Sugar na Ken Gold katika mechi za Nusu Fainali jana.
Azam FC iliwatupa nje waliokuwa mabingwa watetezi, Kagera Sugar kwa kuwachapa 1-0, bao la Ismail Omary Ali kwa penalti dakika ya 75 – baada ya Fountain Gate kuichapa Ken Gold 2-1 hapo hapo Azam Complex.
Safari ya Azam FC katika michuano hii hatua ya Nane Bora ilianzia Kundi A, ambako waliongoza kwa kuvuna ponti saba mbele ya Ken Gold iliyomaliza na pointi sita – hivyo kuzipiku Simba SC iliyomaliza na pointi mbili na Dodoma Jiji washindi wa pili wa msimu uliopita waliomaliza na pointi moja.
Kwa upande wao Fountain Gate waliongoza Kundi B baada ya kuvuna pointi saba, ikiizidi tu wastani wa mabao Kagera Sugar, zote zikizipku Tanzania Prisons iliyomaliza na pointi tatu mna Yanga ambayo ilifungwa mechi zote tatu.

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button