“WATER”
“WATER”
“SAFINA”
“NGANO
“UNGA
“UNGA
HABARI ZA ULAYA

REAL MADRID YAACHANA NA BEKI JESUS VALLEJO BAADA YA MISIMU MITANO

KLABU ya Madrid imeachana na beki Jesús Vallejo Lázaro (28) baada ya misimu mitano ya kuwa na timu hiyo.
Vallejo amekuwa sehemu ya kikosi cha Real Madrid kwa misimu mitano na kushinda mataji LIgi ya Mabingwa Ulaya mawili, Klabu Bingwa ya Dunia ya FIFA mannes, Super Cup ya Ulaya matatu, LaLiga moja, Copa del Rey moja na Super Cup za Hispania mbili.
“Real Madrid ingependa kumshukuru Jesús Vallejo kwa weledi wake, kujitolea, na bidii yake, na inamtakia yeye na familia yake kila la heri katika hatua hii mpya ya maisha yake,”imesema taarifa ya Real Madrid.
Jesús Vallejo Lázaro kisoka aliibukia Zaragoza , kabla ya kusajiliwa Real Madrid mwaka 2015 akiwa ana umri wa miaka 18 na kutolewa kwa mkopo mfululizo Zaragoza, Eintracht Frankfurt, Wolverhampton Wanderers na Granada mara mbili na kuwa mchezaji wa akiba muda wote.
Vallejo alikuwemo kwenye kikosi cha timu ya taifa ya vijana ya Hispania kilichotwaa Kombe la Mataifa ya Ulaya kwa vijana chini ya umri wa miaka 19 ‘Euro Under-21’ mwaka 2019 sambamba na Medali ya Fedha kwenye Michezo ya Olimpiki ya mwaka 2020.

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button