“MARINE”    
“SAFINA”
“NGANO
“UNGA
“UNGA
“WATER”
HABARI MOTOMOTOHABARI ZA NYUMBANI

PAMOJA NA KIKAO NA BODI, YANGA YASISTIZA; “HATUCHEZI”

KLABU ya Yanga imesistiza kutocheza mechi ya marudiano ya Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara dhidi ya watani wao, Simba SC licha ya kikao na Bodi ya Ligi Kuu (TPLB) leo Jijini Dar es Salaam.
Mchezo huo umepangwa kufanyika Jumapili ya Juni 15 kuanzia Saa 11:00 jioni Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam – Yanga wakiwa wenyeji.
Awali mchezo huo ulipangwa kufanyika Machi 8 hapo hapo Uwanja wa Mkapa – lakini TPLB ikaufuta kufuatia Simba kutishia kutoingiza timu ikidai kuzuiwa kufanya mazoezi Machi 7, siku moja kabla ya mechi kwa mujibu wa kanuni.
Bodi ya Ligi ilitangaza rasmi kuuahirisha mchezo huo mchana wa Machi 8, lakini Yanga wakikwenda uwanjani na kufanya mazoezi kabla ya kuondoka na baadaye kufungua kesi Mahakama ya Usuluhishi ya Michezo (CAS).
Hata hivyo CAS ilikataa kusikiliza kesi ya Yanga kutaka ipewe ushindi na kuagiza irejeshe malalamiko yake kwenye mamlaka za nchini. Wakati wa sakata hilo, Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ilikutana na viongozi wa klabu zote, Bodi na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), ingawa haikuwahi kutoa majibu yoyote juu ya mkutano huo uliohudhuriwa pia na viongozi wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT).

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button