“SAFINA”
“NGANO
“UNGA
“UNGA
“WATER”
HABARI ZA AFRIKA MASHARIKI

POLISI BULLETS MABINGWA LIGI YA WANAWAKE KENYA MARA YA PILI MFULULIZO

TIMUya Polisi Bullets imefanikiwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Wanawake kwa mara ya pili mfululizo baada ya ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Trinity Starlets katika mechi ya kuhitimisha msimu Uwanja wa Afraha mjini Nakuru.
Mabao ya Polisi Bullets yalifungwa na Emily Moranga dakika ya 44, Leah Andiema aliyejifunga dakika ya 55 akijaribu kuokoa mpira uliopigwa na Rebecca Okwaro, ambaye alifunga mabao mengine mawii dakika ya 68 na 85.
Mabao mawili aliyofunga jana Rebecca Okwaro yanamfanya awe Mfungaji Bora msimu huu kwa jumla ya mabao yake 16.
Polisi Bullets iliyo chini ya kocha Beldine Odemba inamaliza na pointi 46 baada ya kushinda mechi 13, sare saba na kufungwa moja tu kati ya michezo yote 21 – na sasa itaiwakilisha Kenya katika Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati mwezi Agosti kuwanaia tiketi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Ulinzi Starlets waliokuwa washindani wakuu wa Polisi Bullets kwenye mbio za ubingwa wamemaliza nafasi ya pili kwa pointi zao 44 baada ya ushindi wa 4-0 pia jana Kisumu All Starlets Uwanja wa Ulnzi Sports Complex Jijini Nairobi.

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button