“SAFINA”
“NGANO
“UNGA
“UNGA
“WATER”
HABARI ZA ASIAHABARI ZA KIMATAIFA

CRISTIANO RONALDO ASHINDA TENA KIATU CHA DHAHABU SAUDI ARABIA

MSHAMBULIAJI Mreno, Cristiano Ronaldo kwa mara ya pili mfululizo amekuwa Mfungaji Bora wa Ligi Kuu ya Saudi Arabia na kushinda Kiatu cha Dhahabu Saudi Pro League, huku timu yake ikimaliza nafasi ya tatu katika msimamo wa nyuma ya mabingwa Al Ittihad na Al Hilal waliomaliza nafasi ya pili.
Ronaldo amefunga mabao 25 msimu huu na kuwapiku nyota wa England, Ivan Toney wa Ahli na Mfaransa Karim Benzema wa Al Ittihad – ikiwa ni mwaka mmoja tangu aweke rekodi ya kufunga mabao mengi katika Saudi Pro League alipofunga mabao 35 katika mwechi 31 msimu uliopita.
Katika mechi za mwisho za msimu jana, Ronaldo alifunga bao la kuongoza dakika ya 42, ingawa timu yake, A Nassr ilipoteza mechi kwa kufungwa 3-2 na wenyeji, Al-Fateh Uwanja wa Al Fateh Club mjini Al-Hofuf – hilo likiwa bao lake la 99 katika mechi 111 alizoichezea klabu hiyo yenye maskani yake Riyadh.
Kwa ujumla Ronaldo ambaye aliisaidia Al-Nassr kufika Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa Asia kabla ya kutolewa na Kawasaki Frontale ya Japan ameifungia timu hiyo mabao 35 katika mechi 41 za michuano yote msimu huu, ingawa bahati mbaya, Al-Nassr ilikosa pia mataji ya Super Cup na Kombe la Mfalme Saudi Arabia.
Taji pekee ambalo ameshinda tangu awasili Al Nassri akitokea Manchester United Novemba mwaka 2023 ni Kombe la Klabu Bingwa ya Kiarabu.
Baada ya mchezo wa jana, kumekuwa na uvumi mwingi kuhusu Ronaldo kuondoka baada ya mkataba wake kumalizika mwezi Juni akiwa bado anapambana kufikisha mabao 1,000 ya kufunga kutoka 936 aliyofunga hadi sasa katika maisha yake ya soka.
Mara baada ya mchezo huo, Ronaldo aliandika ujumbe wa siri kwenye X uliosomeka: “Ukurasa huu umekwisha. Historia inaendelea kuandikwa. Asante kwa wote,”.
Rais wa FIFA Gianni Infantino alipendekeza kuwa nyota huyo wa zamani wa Real Madrid na Juventus anaweza kucheza Klabu Bingwa ya Dunai mwezi ujao.

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button