SIMBA SC WASISTIZA KAMA ‘DERBY’ SI JUNI 15 HAWACHEZI SIKU NYINGINE YOYOTE

KLABU ya Simba SC imesema kwamba itapeleka kikosi chake Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara dhidi ya watani, Yanga SC uliopangwa kuanza Saa 11:00 jioni.
Taarifa ya Simba SC jioni hii imesema kwamba itapeleka timu yake uwanjani kwa ajili ya mchezo wa Juni 15 tu na kitakuwa tayari kucheza mechi hiyo tarehe nyingine tofauti na hiyo.
Hadi sasa inafahamika mchezo utafanyika Jumapili ya Juni 15 kwa mujibu wa Bodi ya Ligi ambayo imesistiza hivyo licha ya Yanga kusistiza haitocheza hata baada ya kikao na Bodi ya Ligi Kuu (TPLB) juzi Jijini Dar es Salaam.

Awali mchezo huo ulipangwa kufanyika Machi 8 hapo hapo Uwanja wa Mkapa – lakini TPLB ikaufuta kufuatia Simba kutishia kutoingiza timu ikidai kuzuiwa kufanya mazoezi Machi 7, siku moja kabla ya mechi kwa mujibu wa kanuni.
Bodi ya Ligi ilitangaza rasmi kuuahirisha mchezo huo mchana wa Machi 8, lakini Yanga wakikwenda uwanjani na kufanya mazoezi kabla ya kuondoka na baadaye kufungua kesi Mahakama ya Usuluhishi ya Michezo (CAS).
Hata hivyo CAS ilikataa kusikiliza kesi ya Yanga kutaka ipewe ushindi na kuagiza irejeshe malalamiko yake kwenye mamlaka za nchini. Wakati wa sakata hilo, Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ilikutana na viongozi wa klabu zote, Bodi na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), ingawa haikuwahi kutoa majibu yoyote juu ya mkutano huo uliohudhuriwa pia na viongozi wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT).
Yanga imekwenda mbali na kutishia kususia hata mechi nyingine mbili za kumalizia msimu dhidi ya Tanzania Prisons na Dodoma Jiji pamoja na kujitoa kwenye Ligi ya msimu ujao wapo matakwa yao matatu Kati ya manne hayatatimizwa.
Matakwa hayo ni Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi ijiuzulu, Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi Almasi Kasongo ajiuzulu,Katibu Mkuu wa TFF, Wilfred Kidao naye ajiuzulu — na la nne ambalo ni la muda mrefu nyundo mpya wa Bodi Huru ya Ligi.