JKT TANZANIA YAICHAPA FOUNTAIN GATE 3-1 MBWENI
TIMU ya JKT Tanzania imeibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Fountain Gate kwenye Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Meja Jenerali Charles Isamuhyo, Mbweni Jijini Dar es Salaam.
Mabao ya JKT Tanzania yamefungwa na Mohamed Bakari dakika ya saba, Shiza Kichuya dakika ya 45 na Edward Songo dakika ya 59, wakati bao pekee la Fountain Gate limefungwa na Edgar William dakika ya 87.
Kwa ushindi huo, JKT Tanzania inafikisha pointi 35 na kusogea nafasi ya sita, wakati Fountain Gate inabaki na pointi zake 29 nafasi ya 13 kwenye ligi ya timu 16.
Tayari Kagera Sugar na Ken Gold zimeshuka daraja, wakati timu zitakazomaliza nafasi ya 14 na 13 zitamenyana katika Play-Off kwa mechi mbili za nyumbani na ugenini na mshindi wa jumla atabaki Ligi Kuu, wakati timu itakayotolewa itakwenda kucheza timu kutoka Championship kujaribu tena kubaki Ligi Kuu.
Kutoka Championship Mtibwa Sugar imepanda Ligi Kuu kama bingwa ikiungana na washindi wa pili, Mbeya City – wakati Ken Gold na Stand United zilizomaliza nafasi ya tatu nan ne ndizo zitakazomenyana katika Play-Off kuwania kucheza na timu itakayoporomoka Ligi Kuu kujaribu tena kupanda Ligi Kuu.