“SAFINA”
“NGANO
“UNGA
“UNGA
“WATER”
HABARI ZA KIMATAIFAHABARI ZA ULAYA

SPURS WAIPIGA MAN UNITED 1-0 NA KUTWAA TAJI LA UEFA EUROPA LEAGUE

TIMU ya Tottenham Hotspur imemaliza ukame wa mataji wa miaka 17 kwa kutwaa Kombe la UEFA Europa League baada ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Manchester United usiku wa jana Uwanja wa San Mamés Barria Jijini Bilbao nchini Hispania.
Shujaa wa Spurs ni mshambuliaji wa Kimataifa wa Wales, Brennan Price Johnson (23) aliyefunga bao hilo pekee dakika ya 42 akimalizia krosi ya kiungo Msenegal, Pape Matar Sarr (22), ushindi ambao unanipa pia Tottenham tiketi ya kucheza UEFA Champions League msimu ujao licha ya kufanya vibaya msimu huu England.
Ni furaha kwa Kocha Mkuu wa Spurs, Muaustralia, Ange Postecoglou ambaye ahadi yake ya kuipa timu taji ndani ya misimu miwili ya kwanza kazini imetimia.
Ni taji la nne la michuano hii kwa Spurs baada ya awali kulitwaa misimu ya 1971–72, 1983–84 enzi za UEFA Cup na 2024–25, wakati taji lingine la Ulaya walilowahi kutwaa ni UEFA Cup Winners’ Cup mara moja, 1962–63.
Zaidi ya hapo wana mataji nane ya FA Cup waliyotwaa 1900–01, 1920–21, 1960–61, 1961–62, 1966–67, 1980–81, 1981–82 na 1990–91, manne ya Kombe la Ligi 1970–71, 1972–73, 1998–99 na 2007–08 na Ngao ya Jamii mara saba 1921, 1951, 1961, 1962, 1967, 1981 na 1991.

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button