“WATER”
“WATER”
“SAFINA”
“NGANO
“UNGA
“UNGA
HABARI MOTOMOTOHABARI ZA AFRIKAHABARI ZA NYUMBANI

HABARI ZA NYUMBANI

BINGWA wa Kombe la Shirikisho Afrika mwaka huu atapewa Kombe jipya kama ilivyo katika Ligi ya Mabingwa Afrika, ambayo yatazinduliwa Alhamisi (Mei 22, 2025) katika ofisi za wadhamini wakuu, TotalEnergies Jijini Johannesburg, Afrika Kusini.
Hafla ya uzinduzi wa mataji hayo itaanza Saa 12:00 jioni na itahudhuriwa na magwiji wa soka barani Afrika na klabu zinakazomenyana katika Fainali ya Ligi ya Mabingwa, Mamelodi Sundowns na Pyramids FC.  
Mchezo wa marudiano wa Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika utafanyika Jumapili wiki hii kuanzia Saa 10:00 jioni Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar – Simba SC wakiwa wenyeji wa RSB Berkane ya Morocco.
Mchezo wa kwanza uliofanyika Jumamosi iliyopita (Mei 17, 2025) Uwanja wa Manispaa ya Berkane mjini Berkane nchini Morocco – wenyeji, RSB Berkane walishinda 2-0 mabao ya kiungo Msenegal, Mamadou Lamine Camara dakika ya nane na mshambuliaji Oussama Lamlaoui la pili dakika ya 14.
Fainali ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika itachezwa Jumamosi, (Mei 24, 2025), Mamelodi Sundowns kuanzia Saa 10:00 jioni Uwanja wa Loftus Versfeld Jijini Pretoria, Afrika Kusini na marudiano yatafuatia Juni 1 Uwanja wa Jeshi la Anga wa Juni 30Jijini Cairo, Misri. 

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button