“SAFINA”
“NGANO
“UNGA
“UNGA
“WATER”
HABARI ZA NYUMBANI

ENEKIA KASONGA ‘LUNYAMILA’ AHAMIA TIMU NYINGINE MEXICO

KIUNGO mshambuliaji wa Kimataifa wa Tanzania, Enekia Kasonga ‘Lunyamila’ (23) amejiunga na klabu ya FC Juárez akitokea Mazatlán, zote za Ligi Kuu ya Wanawake nchini Mexico ‘Liga MX Femenil’.
Enekia ametambulishwa asmi kuwa mchezaji mpya wa FC Juarez akiungana na Watanzania wenzake wawili, beki Julitha Singano na mshambuliaji, Opa Clement wanaochezea klabu hiyo pia.
Eenekia aliyezaliwa Kigoma Aprili 20, mwaka 2002, kisoka aliibukia Alliance FC ya Mwanza mwaka 2016, kabla ya kujiunga na Ruvuma Queens mwaka 2018 alikocheza hadi mwaka 2021 Ausfaz Assa-Zag ya Morocco.


Mwaka 2023 alihamia Ausfaz Assa-Zag ya Ukraine alikocheza hadi 2023 alipohamia Eastern Flames ya Saudi Arabia aliyoichezea hadi alipohamia Mazatlán mwaka jana.
Amekuwa mchezaji wa timu ya taifa tangu mwaka 2018 baada ya kupandishwa kutoka timu ya vijana chini ya umri wa miaka 20 na hadi sasa ameichezea Twiga Stars mechi 28 na kufunga mabao 20.
Kwa sasa yupo kambini Dar es Salaam kwenye kikosi cha Twiga Stars kinachojiandaa naFainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Wanawake (WAFCON) zinatarajiwa kufanyika nchini Morocco kuanza Julai 5 hadi 26, mwaka huu.


Na jana alikuwa sehemu ya kikosi cha Twiga Stars kilichoibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) ‘Léopards Dames’ katika mchezo wa kirafiki leo Uwanja wa Azam Complex Chamazi, Dar es Salaam.
Mabao ya Twiga Stars yalifungwa na wachezaji wenzake wa FC Juárez ya Mexico, Opah Clement dakika ya 26, beki Julitha Singano dakika ya 43 – lingine likifungwa na kiungo mshambuliaji wa Al Nassr ya Saudi Arabia, Clara Luvanga dakika ya 47, wakati bao pekee la DRC lilifungwa na mshambuliaji wa TP Mazembe ya kwao, Lubumbashi Esther Dikisha dakika ya 90.
Ulikuwa mchezo wa pili kuzikutanisha timu hizo ndani ya tano, baada ya Ijumaa pia Twiga Stars kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 hapo hapo Azam Complex, mabao ya Twiga Stars yote yakifungwa na Clara Luvanga dakika ya 28 na 88, wakati bao pekee la Léopards Dames lilifungwa na Esther Dikisha dakika ya 72.
Tanzania imepangwa Kundi C pamoja na Afrika Kusini, Ghana na Mali, wakati DRC ipo Kundi A pamoja na wenyeji, Morocco, Zambia na Senegal na Kundi B kuna Nigeria, Tunisia, Algeria na Botswana.

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button