INDIANA PACERS YAICHAPA OKLAHOMA CITY THUNDER 111-110 GAME 1 FAINALI NBA 2025

TIMU ya Indiana Pacers imetoka nyuma kwa pointi 15 katika quarter ya nne na kuibuka na ushindi wa pointi 111-110 dhidi ya Oklahoma City Thunder katika Game 1 ya Fainali za NBA 2025 usiku wa kuamkia leo ukumbi wa Paycom Center, Oklahoma City, Oklahoma.
Shujaa wa Indiana Pacers ni Tyrese Haliburton ambaye kwa mara nyingine alifunga pointi za ushindi zikiwa zimebaki sekunde 0.3 akirudia alichokifanya dhidi ya Milwaukee Bucks, Cleveland Cavaliers kuipa ushindi timu yake na kwenye Fainali ya Eastern Conference dhidi ya New York Knicks.
Haliburton alimaliza na pointi 14, rebounds 10 na assists sita katika ushindi huo wa kutkea nyuma ambao ulishuhudia wachezaji sita tofauti wa Pacers wakipiga alama kuanzia 10 (double figures) na wote zisizozidi pointi 19.
Huo ulikuwa uongozi wa kwanz akwa Indiana kwenye mchezo huo na ukatosha wa kuwapa ushindi sekunde 0.3 za mwisho na kuzima juhudi za MVP wa Ligi, Shai Gilgeous-Alexander aliyefunga pointi 38, rebounds tano, assists tatu na steals tatu.
Game 2 itafuatia Jumamosi ya Juni 8 hapo hapo Paycom Center, Oklahoma City, Oklahoma, Game 3 Juni 11 na Game 4 Juni 13 zote zitahamia Gainbridge Fieldhouse, Indianapolis.