“MARINE”    
“SAFINA”
“NGANO
“UNGA
“UNGA
“WATER”
HABARI ZA KIMATAIFAHABARI ZA ULAYA

NI URENO YA RONALDO BINGWA LIGI YA ULAYA

URENO imefanikiwa kutwaa taji la Ligi ya Mataifa ya Ulaya baada ya ushindi wa Penalti 5-3 dhidi ya Hispania usiku wa kuamkia leo Uwanja wa Allianz Arena Jijini Munich nchini Ujerumani.
Haukuwa ushindi mwepesi kwa Ureno, kwani ndani ya dakika 90 ililazimika kutoka nyuma mara mbili ili kupata sare ya 2-2, huku Mwanasoka Bora wa zamani wa Dunia, Cristiano Ronaldo akiinusuru timu hiyo kupotezwa mapema.
Mbele ya watazamaji 65,852 kiungo wa Real Sociedad, Martín Zubimendi alianza kuifungia Hispania dakika ya 21, kabla ya beki wa kushoto wa Paris Saint-Germain, Nuno Mendes kuisawazishia Ureno dakika ya 26.
Nyota mwenzake wa Real Sociedad, mshambuliaji Mikel Oyarzabal akawatanguliza tena La Roja dakika ya 45 – lakini mkongwe, Ronaldo akaisawazishia A Seleção das Quinas dakika ya 61.
Ililuwa ni mechi nzuri iliyowakutanisha nyota wawili gumzo, Cristiano Ronaldo na chipukizi, Lamine Yamal katika usiku ambao muda wa kuamua bingwa wa UEFA Nations League 2025 ulipowadia wote wawili walikuwa benchi.
Ronaldo, mkongwe wa umri wa miaka 40 — alitolewa dakika ya 88 baada ya kuumia misuli nafasi yake ikichukuliwa na Gonçalo Ramos na Yamal, kinda wa miaka 17 alipumzishwa dakika ya 105 nafasi yake ikichukuliwa na Yeremy Pino.
Kipa wa FC Porto ya nyumbani,
Diogo Costa aliokoa mkwaju wa penalti wa mkongwe Alvaro Morata, kabla ya kiungo wa Paris Saint-Germain, Rúben Neves kuifungia Ureno penalti ya mwisho ya ushindi.
Wengine waliifunga penalti za Ureno ni mshambuliaji, Gonçalo Ramos, kiungo Vitinha na Nuno Mendes wote wa Paris Saint-Germain na kiungo wa Manchester United, Bruno Fernandes.
Waliofunga penalti za Hispania ni viungo, Mikel Merino wa Arsenal, mshambuliaji, Álex Baena wa Villarreal na Isco wa Real Betis.
Hilo taji la pili la michuano hiyo kwa Ureno baada ya kuweka rekodi ya kuwa mabingwa wa kwanza wa michuano hiyo mwaka 2019 na kuipiku Hispania ambayo pia ilikuwa ina taji moja la mwaka 2023.

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button