“SAFINA”
“NGANO
“UNGA
“UNGA
“WATER”
HABARI ZA AFRIKA

PYRAMIDS YATWAA TAJI LA KWANZA LIGI YA MABINGWA AFRIKA

WENYEJI, Pyramids FC wamefanikiwa kutwaa taji lao la kwanza la Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini katika mchezo wa marudiano was Fainali usiku huu Uwanja wa Jeshi la Anga wa Juni 30 Jijini Cairo nchini Misri.
Pyramids wanatwaa ubingwa wa Afrika kwa ushindi wa jumla wa 3-2 kufuatia sare ya 1-1 kwenye mchezo wa kwanza wiki iliyopita Jijini Pretoria na kuwa klabu ya nne ya Misri kuwahi kutwaa taji hilo — nyingine Al Ahly, Zamalek, na Ismailia.
Mabao ya Pyramids yamefungwa na mshambuliaji wa Kimataifa was Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Fiston Kalala Mayele dakika ya 23 na beki Mmisri, Ahmed Samy Saad dakika ya 56, wakati bao pekee la Mamelodi Sundwons limefungwa na mshambuliaji mzawa, Iqraam Rayners dakika ya 75.

Matokeo hayo yanaashiria mara ya kwanza Pyramids kunyanyua taji la bara, muongo mmoja baada ya kuanzishwa kwa klabu hiyo huku pia ikilibakiza taji hilo Misri kwa mwaka wa tatu mfululizo kufuatia ushindi wa Al Ahly mwaka 2023 na 2024.
Kwa Sundowns, ambao walikuwa wakisaka taji hilo kwa mara ya pili ili kuwa timu ya kwanza tangu Al Ahly mwaka 2012 kushinda baada ya kushindwa kupata ushindi katika mechi ya nyumbani kwenye fainali.
Badala yake, Wabrazil hao wanapata kipigo chao cha pili katika fainali ya Ligi ya Mabingwa, miaka 24 baada ya kushindwa na Al Ahly mwaka 2001.

WAFUNGAJI BORA WA MABAO

RankPlayerTeamMD1MD2MD3MD4MD5MD6QF1QF2SF1SF2F1F2Total
1 Fiston Mayele Pyramids12216
2 Ibrahim Adel Pyramids2125
 Emam Ashour Al Ahly131
4 Relebohile Mofokeng Orlando Pirates11114
 Mohau Nkota Orlando Pirates211

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button