“WATER”
“WATER”
“SAFINA”
“NGANO
“UNGA
“UNGA
HABARI ZA AFRIKAHABARI ZA NYUMBANI

PAMBA YAICHAPA KEN GOLD 2-0 NA KUISHUSHA DARAJA KAGERA SUGAR

USHINDI wa mabao 2-0 wa Pamba Jiji FC dhidi ya wenyeji, Ken Gold Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya jioni ya leo unahitimisha ushiriki wa Kagera Sugar kwenye Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara.


Mabao yote ya Pamba Jiji yamefungwa na mshambuliaji Mguinea, Abdoulaye Yonta Camara dakika ya 30 na 60 na kwa ushindi huo wanafikisha pointi 30 katika mchezo wa 28, ambazo Kagera Sugar hawawezi kufikisha hata wakishinda mechi zao zoite mbili zilizosalia.


Pamba wanasogea nafasi ya 11 wakizizidi tu wastani wa mabao Tanzania Prisons iliyocheza mechi 28 pia na KMC iliyocheza mechi 27, wakati Kagera Sugar wanabaki nafasi ya 15 kwa pointi zao 22 mbele ya Ken Gold inayoshika mkia kwa pointi zake 17 baada ya wao pia kucheza mechi 28.


Kagera Sugar wanaungana na Ken Gold iliyokuwa ya kwanza kushuka daraja, wakati timu zitakazomaliza nafasi ya 14 na 13 zitamenyana katika Play-Off kwa mechi mbili za nyumbani na ugenini na mshindi wa jumla atabaki Ligi Kuu, wakati timu itakayotolewa itakwenda kucheza timu kutoka Championship kujaribu tena kubaki Ligi Kuu.


Kutoka Championship Mtibwa Sugar imepanda Ligi Kuu kama bingwa ikiungana na washindi wa pili, Mbeya City – wakati Ken Gold na Stand United zilizomaliza nafasi ya tatu nan ne ndizo zitakazomenyana katika Play-Off kuwania kucheza na timu itakayoporomoka Ligi Kuu kujaribu tena kupanda Ligi Kuu.

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button