HABARI MOTOMOTOHABARI ZA NYUMBANI
UCHAGUZI MKUU TFF KUFANYIKA AGOSTI 16 TANGA

UCHAGUZI Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) umepangwa kufanyika Agosti 16, mwaka huu Jijini Tanga.
Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya TFF, Wakili Kiomoni Kibamba amewaambia Waandishi wa Habari leo Jijini Dar es Salaam kwamba nafasi zitakazogombewa ni Urais nafasi moja na Wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya sita.
Wakili Kibamba amesema gharama ya fomu ya Urais ni Sh. 500,000 na za Ujumbe wa Kamati ya Utendaji Fomu inatolewa kwa gharam ya Sh 200,000.
Wakili Kibamba amesema kwamba zitaanza kutolewa Jumatatu ya Juni 16, 2025 Saa 10:00 makao makuu ya TFF, Uwanja wa Karume, Ilala Jijini Dar es Salaam na kwenye tovuti ya shirikisho hilo.


