“SAFINA”
“NGANO
“UNGA
“UNGA
“WATER”
HABARI ZA NYUMBANI

CLARA AFUNGA MAWILI TWIGA STARS YAICHAPA DRC 2-1 CHAMAZI

TIMU ya taifa ya wanawake ya Tanzania ‘Twiga Stars’ imeibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) ‘Léopards Dames’ katika mchezo wa kirafiki leo Uwanja wa Azam Complex Chamazi, Dar es Salaam.
Mabao yote ya Twiga Stars yamefungwa na mshambuliaji wa Al Nassr ya Saudi Arabia, Clara Cleitus Luvanga dakika ya 28 na 88, wakati bao pekee la Léopards Dames limefungwa na mshambuliaji Esther Dikisha Bushiri wa TP Mazembe ya kwao, Lubumbashi dakika ya 72.
Timu hizi zitarudiana tena Juni 3 hapo hapo Azam Complex – hayo yakiwa maandalizi ya Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Wanawake (WAFCON) kwa timu zote zinazotarajiwa kuanza Julai 5 hadi 26, mwaka huu nchini Morocco.
Tanzania imepangwa Kundi C pamoja na Afrika Kusini, Ghana na Mali, wakati DRC ipo Kundi A pamoja na wenyeji, Morocco, Zambia na Senegal na Kundi B kuna Nigeria, Tunisia, Algeria na Botswana.

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button