“MARINE”    
“SAFINA”
“NGANO
“UNGA
“UNGA
“WATER”
HABARI ZA KIMATAIFA

JAMAL MUSIALA APIGA HAT-TRICK BAYERN YASHINDA 10-0 KOMBE LA DUNIA

TIMU ya Bayern Munich ya Ujerumani imeibuka na ushindi wa mabao 10–0 dhidi ya Auckland City ya New Zealand katika mchezo wa Kundi C Kombe la Klabu Bingwa ya Dunia ya FIFA usiku huu Uwanja wa TQL, Cincinnati, Hamilton County, Ohio, Marekani.
Mbele ya mashabiki 21,152, kiungo Mjerumani mwenye asili ya Nigeria, Jamal Musiala ameweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza kufunga hat-trick kwenye michuano hiyo kwa mabao yake ya dakika za 67, 73 kwa penalti na 84.
Nao mawinga Wafaransa walifunga mabao mawili kila mmoja, Kingsley Junior Coman dakika ya sita na 21 na Michael Akpovie Olise mzaliwa wa England mwenye asili ya Nigeria dakika ya 20 na 45’+3 kama ilivyokuwa kwa kiungo mkongwe Mjerumani, Thomas Müller dakika ya 45 na 89.
Katika mchezo huo uliochezeshwa na refa Msenegal, Issa Sy — bao lingine la The Bavarians limefungwa na beki Mfaransa mwenye asili ya Cameroon, Sacha Boey dakika ya 18.

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button