“MARINE”    
“SAFINA”
“NGANO
“UNGA
“UNGA
“WATER”
HABARI ZA AMERIKA

LIONEL MESSI MCHEZAJI BORA WA MWEZI MEI LIGI YA MAREKANI

NAHODHA wa Inter Miami CF Lionel Messi amechaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa Mwezi Mei, mwaka 2025 wa Ligi Kuu ya Marekani (MLS).
Messi ameshinda tuzo hiyo baada ya kuonyesha kiwango kikubwa mwezi Mei, akifunga mabao saba na kuongeza pasi nne za mabao hivyo kuongoza katika ligi ya MLS kwa kuchangia mabao 11 huku Inter Miami ikimaliza mwezi huo bila kupoteza mechi kati ya tatu ilizocheza.
Na ushindi huo unakuja baada ya nyota huyo wa Argentina kushinda mfululizo Tuzo za Mchezaji Bora wa Mechi akikabidhiwa na Michelob Ultra.
Katika Raundi ya 16 ya mechi za MSL, Messi alifunga mabao mawili na kutoa pasi mabao bao moja Inter Miami ikishinda 4-2 dhidi ya CF Montréal akiirejesha timu yake kwenye njia za ushindi.
Kiwango hicho pia kilimfanya Messi kuwa mchezaji wa kwanza katika historia ya klabu hiyo kuchangia mabao 50 katika msimu mmoja akiw aamefunga jumla ya mabao 31 na kutoa pasi za mabao 24 katika mechi 38 pekee.
Jumamosi iliyopita, Messi alionyesha kiwango bora mno katika ushindi wa 5-1 dhidi ya wapinzani wao wa Kanda ya Mashariki, Columbus Crew, akichangia kila bao la Inter Miami huku akifunga mara mbili na kuongeza pasi tatu za mabao.

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button