“WATER”
“WATER”
“SAFINA”
“NGANO
“UNGA
“UNGA
HABARI ZA AFRIKA MASHARIKI

APR MABINGWA WA RWANDA KWA MARA YA SITA MFULULIZO NA 23 JUMLA


WENYEJI, APR jana walifanikiwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Rwanda kwa mara ya sita mfululizo kufuatia ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Muhazi United katika mchezo uliofanyika Uwanja wa Ngoma mjini Kubungo.
Pongezi kwa mfungaji wa bao hilo pekee, mshambuliaji Mburkinabe, Cheikh Djibril Ouatarra na hilo linakuwa taji lao la 23 jumla na la sita mfululizo tangu mwaa 2020, baada ya Rayon Sports kushindwa kuifunga Vision FC iliyoshuka daraja kwenye Uwanja wa Pele Jijini Kigali wakitoka sare tasa.
APR walikuwa na safu zao kamili za ushambuliaji uwanjani ikiongozwa na Mchezaji Bora wa Mwaka Ouatarra sambamba na Denis Omedi na Gilbert Mugisha.
Matokeo hayo yalitosha kunyakua taji hilo kwani walitangulia kwa pointi nne wakiwa na pointi 64 mbele ya Rayon walio na pointi 60.
Matumaini ya The Blues kutwaa ubingwa yalimalizika baada ya kulazimishwa sare ya 0-0 dhidi ya Vision, ingawa timu hiyo haikupigania chochote.
Vision FC ilibidi wacheze dakika tano za mwisho za mchezo wakiwa pungufu baada ya Michael Lutaya kutolewa nje kwa kadi nyekundu, lakini vijana wa Claude Rwaka walishindwa kutumia nafasi hiyo kupata mabao.

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button