“MARINE”    
“SAFINA”
“NGANO
“UNGA
“UNGA
“WATER”
HABARI ZA NYUMBANI

AZAM FC YAMSAJILI MSHAMBULIAJI ALIYEPANDISHA TIMU LIGI KUU MISRI

KLABU ya Azam FC imemtambulisha mshambuliaji Mtanzania Muhsini Malima Makame (24) aliyekuwa anacheza Misri kuwa mchezaji wake mpya kuelekea msimu ujao kwa mkataba wa mwaka mmoja.
Malima aliyekuwa anachezea klabu ya Zed FC tangu ikiwa Daraja la Kwanza hadi inapanda msimu uliopita anakuwa mchezaji mpya wa pili tu kutambulishwa kuelekea msimu ujao baada ya beki Lameck Elias Lawi kutoka Coastal Union ya Tanga.
Malima ameibuka pamoja na mchezaji mwingine wa Azam FC, kiungo mshambuliaji Abdul Suleiman ‘Sopu’ katika timu ya vijana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys mwaka 2017.

Baada ya kufanya vizuri katika Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa vijana chini ya miaka 17 (AFCON U17) mwaka 2017 nchini Gabon — Malima alielekeza nguvu zake kwenye kutafuta timu za kuxhezea Ulaya.
Alianzia Serbia katika timu ya vijana U19 ya Red Star Belgrade mwaka 2020, ambayo baada ya kumsajili ilimpeleka kwa mkopo Graficar ya huko pia na mwishoni mwa msimu alipomaliza mkataba akarejea nyumbani.
Hapa nchini alichezea klabu za Coastal Union msimu wa 2020-2021 na Dodoma Jiji FC msimu wa 2022-2023, kabla ya kwenda Misri kujiunga na Zed FC Agosti 13, mwaka 2023 hadi sasa anarejea nchini kwa ajili ya Azam FC.

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button