“WATER”
“WATER”
“SAFINA”
“NGANO
“UNGA
“UNGA
HABARI MOTOMOTOHABARI ZA NYUMBANI

YANGA YAICHAPA NAMUNGO FC 3-0 MWENGE

MABINGWA watetezi, Yanga SC wameibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Namungo FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, KMC Complex, Mwenge, Dar es Salaam.


Mabao ya Yanga leo yamefungwa na Mburkinabe, Stephane Aziz Ki dakika ya 27, Mzimbabwe Prince Dube Mpumelelo dakika ya 31 na Mkongo, Maxi Mpia Nzengeli dakika ya 74.


Kwa ushindi huo, Yanga wanafikisha pointi 73 katika mchezo wa 28 na kuendelea kuongoza Ligi Kuu kwa pointi nne zaidi ya wapinzani wao kwenye mbio za ubingwa, Simba SC ambao pia wana mechi moja mkononi.


Kwa upande wao Namungo FC baada ya kupoteza mchezo wa leo wanabaki na pointi 31 baada ya kucheza mechi 28 pia wakiwa nafasi ya 10, kwenye ligi ya timu 16 ambayo mwisho wa msimu mbili zitashuka daraja.


Tayari Kagera Sugar na Ken Gold zimeshuka daraja, wakati timu zitakazomaliza nafasi ya 14 na 13 zitamenyana katika Play-Off kwa mechi mbili za nyumbani na ugenini na mshindi wa jumla atabaki Ligi Kuu, wakati timu itakayotolewa itakwenda kucheza timu kutoka Championship kujaribu tena kubaki Ligi Kuu.


Kutoka Championship Mtibwa Sugar imepanda Ligi Kuu kama bingwa ikiungana na washindi wa pili, Mbeya City – wakati Ken Gold na Stand United zilizomaliza nafasi ya tatu nan ne ndizo zitakazomenyana katika Play-Off kuwania kucheza na timu itakayoporomoka Ligi Kuu kujaribu tena kupanda Ligi Kuu.

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button