“MARINE”    
“SAFINA”
“NGANO
“UNGA
“UNGA
“WATER”
HABARI ZA AFRIKA

NI RSB BERKANE MABINGWA KOMBE LA SHIRIKISHO 2024-2025

TIMU ya Renaissance Sportive de Berkane ya Morocco imefanikiwa kutwaa Kombe la Shirikisho Afrika 2024-2025 baada ya sare ya kufungana bao 1-1 na wenyeji, Simba SC katika mchezo wa marudiano wa Fainali jioni ya leo Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar.
Kwa matokeo hayo, RSB Berkane inatwaa Kombe hilo kwa ushindi wa jumla wa 3-1 kufuatia kushinda mabao 2-0 kwenye mchezo wa kwanza Jumamosi iliyopita Uwanja wa Manispaa ya Berkane mjini Berkane.
Kwa kutwaa taji hilo, RSB Berkane wamesahihisha makosa yao ya Fainali ya msimu uliopita walipozidiwa kete na Zamalek kwa kuruhusu bao nyumbani baada ya mchezo kumalizika kwa sare ya jumla ya 2-2, wakishinda 2-1 Morocco na kwenda kufungwa 1-0 Misri.
Katika mchezo wa leo Simba SC walitangulia kwa bao la Mzambia, Joshua Mutale Budo dakika ya 17 akimalizia pasi ya winga mwenzake, Mkongo Elie Mpanzu Kibisawala – kabla ya kiungo wa Kimataifa wa Mali, Soumaila Sidibe kuisawazishia RSB Berkane dakika ya 90’+3.
Hii inakuwa mara ya tatu kwa RSB Berkane kutwaa CAF Confederation Cup baada ya mwaka 2020 na 2022, mwaka ambao pia walitwaa taji la CAF Super Cup.
Pamoja na kupewa Kombe jipya, RSB Berkane wanapatiwa kitita cha Dola za Kimarekani Milioni 2, huku washindi wa pili, Simba SC wakipata Dola Milioni 1.

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button