“MARINE”    
“SAFINA”
“NGANO
“UNGA
“UNGA
“WATER”
HABARI ZA ULAYA

KEVIN DE BRUYNE AJIUNGA NA NAPOLI KWA MKATABA WA MIAKA MIWILI

KLABU ya Napoli ya Itali imemsajili kiungo mkongwe wa Kimataifa wa Ubelgiji, Kevin De Bruyne kama mchezaji huru baada ya kumaliza mkataba wake Manchester City mapea mwezi huu, Juni.
Kevin De Bruyne amekubali kusaini mkataba wa miaka miwili na mabingwa hao wa Serie A wenye kipengele cha kuongeza mwaka wa tatu, kwa mujibu wa taarifa ya mwandishi nguli wa habari wa Italia, Gianluca Di Marzio.
De Bruyne, anayechukuliwa kuwa mmoja wa wachezaji bora wa kizazi chake anahamia Italia baada ya muongo mmoja wa mafanikio makubwa England akiwa na Manchester City ambayo ameifungia mabao 108 na pasi za mabao 177 katika mechi 422 kwenye kikosi cha Kocha Mspaniola, Pep Guardiola.
Katika utumishi wake Uwanja wa Etihad, Kevin De Bruyne ameshinda mataji sita ya Ligi Kuu, mawili ya Kombe la FA, matano ya Kombe la Ligi, matatu ya Ngao ya Jamii na moja la Ligi ya Mabingwa mwaka 2023.
Kevin De Bruyne (33) anajiunga na Napoli ambayo imetwaa taji la Serie A chini ya Kocha Antonio Conte msimu wa 2024-25, likiwa ni taji lao la pili ndani ya miaka mitatu.

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button