“MARINE”    
“SAFINA”
“NGANO
“UNGA
“UNGA
“WATER”
HABARI ZA NYUMBANI

KOMBE LA CECAFA CHALLENGE WANAWAKE KUFANYIKA CHAMAZI JUNI 12 HADI 22

MICHUANO ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati kwa Wanawake (CECAFA Womens Challenge Cup) inatarajiwa kufanyika kuanzia Juni 12 hadi 22, mwaka huu Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Mashindano wa Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA), Yusuf Mossi amesema kwamba iliamuliwa kuwa mashindano hayo yafanyike kabla ya michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Wanawake (WAFCON) mwezi ujao nchini Morocco.
“Mashindano hayo yatasaidia wawakilishi wetu wa WAFCON Tanzania kujiandaa vyema na timu nyingine pia kujiandaa na mchujo wa WAFCON 2026 utakaorejea Oktoba mwaka huu,”aliongeza Mossi.
Aliweka wazi kuwa tayari wenyeji Tanzania, Uganda, Burundi na Sudan Kusini wamethibitisha kushiriki, huku timu zaidi zikitarajiwa kuthibitisha siku chache zijazo.


Baada ya Mashindano ya Wakubwa ya Wanawake, Mashindano ya kwanza ya CECAFA ya Soka ya Ufukweni yatafuatia kuanzia Julai 7 hadi 12 mjini Mombasa nchini Kenya.
Mashindano mengine ya CECAFA mwaka huu ni Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, ‘Dar Port Kagame Cup’ yatakayofanyika Darv es Salaam, Tanzania, michuano ya kufuzu Fainali za Afrika kwa vijana chini ya umri wa miaka 17 (AFCON U-17) itakayofanyika nchini Ethiopia na kufuzu kwa Michuano ya Ubingwa wa Shule za Afrika.
Taarifa ya CECAFA imesema kwamba michuano ya wakubwa kwa wanaume CECAFA Challenge Cup na a wasichana chini ya umri wa miaka 20 haitafanyika mwaka huu.

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button