“SAFINA”
“NGANO
“UNGA
“UNGA
“WATER”
HABARI MOTOMOTOHABARI ZA NYUMBANI

YANGA YAMUAGA RASMI STEPHANE AZIK KI

KLABU ya Yanga imemuaga kiungo wake mshambuliaji Mburkinabe mzaliwa wa Ivory Coast, Stephane Aziz Ki baada ya misimu mitatu ya kuwa naye tangu awasili kutoka ASEC Mimosas.
Taarifa zinasema Aziz Ki anakwenda kujiunga na Wydad Athletic ya Morocco na usajili wake umeharakishwa ili akacheze michuano ya Klabu Bingwa ya Dunia ya FIFA.
Aziz alijiunga na Yanga Julai mwaka 2022 akitokea ASEC Mimosas ambayo aliichezea kuanzia Januari mwaka 2021 alipowasili akitokea
AFAD Djékanou ya Ivory Coast pia.
Kisoka Azi Ki alianzia timu za vijana za Hispania, Rayo U19 mwaka 2015 na San Roque Lepe mwaka 2016, kabla ya kwenda Cyprus ambako alichezea Omonia Nicosia kuanzia 2016 hadi 2017, ingawa katikati alipelekwa kwa mkopo Aris Limassol ya huko pia.
Mwaka 2018 alijiunga na Nea Salamis ya Cyprus pia hadi 2019 aliporudi Ivory Coast na kuchezea AFAD Djékanou na ASEC kabla ya kuja Tanzania kujiunga na Yanga.
Katika misimu yake mitatu ya kuwa Yanga amecheza jumla ya mechi rasmi 114 na kufunga mabao 57 na pasi za mabao 32, akishinda jumla ya mafaji nane, Ligi Kuu, Kombe la TFF na Ngao ya Jamii yote mara mbili pamoja na Kombe la Muungano na Kombe la Toyota.
Msimu uliopita, 2023-2024 ulikuwa wa mafanikio zaidi kwake akitwaa Tuzo za Mfungaji Bora, Mchezaji Bora na Kiungo Bora wa Ligi Kuu pamoja na kuiongoza Yanga kuwafunga watani, Simba SC 5-1.
Zaidi ya mafanikio ya ndani ya Uwanja, Aziz Ki pia amepata mke Tanzania, amemuoa Mwanamitindo Hamisa Mobetto na hivi sasa tayari yupo naye Ivory Coast.

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button