• HABARI MPYA

  Jumanne, Januari 04, 2022

  WOLVES YAICHAPA MAN UNITED 1-0 OLD TRAFFORD


  WENYEJI, Manchester United wamechapwa 1-0 na Wolverhampton Wanderers katika mchezo wa Ligi Kuu ya England usiku wa Jumatatu Uwanja wa Old Trafford, bao pekee la Joao Moutinho dakika ya 82.
  Nahodha wa leo, Cristiano Ronaldo aliifungia bao la kichwa Manchester United mwishoni mwa mchezo ambao lingekuwa la kusawazisha, lakini akaambiwa alikuwa ameotea.
  Kwa ushindi huo, Wolves inafikisha pointi 28 katika nafasi ya nane, sasa inazidiwa tatu na Manchester United wanaoshika nafasi y saba baada ya wote kucheza mechi 19.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: WOLVES YAICHAPA MAN UNITED 1-0 OLD TRAFFORD Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top