• HABARI MPYA

  Jumapili, Januari 02, 2022

  CHELSEA YAAMBULIA SARE KWA LIVERPOOL, 2-2 DARAJANI


  WENYEJI, Chelsea wametoka nyuma kwa mabao 2-0 na kupata sare ya 2-2 na Liverpool katika mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa Stamford Bridge Jijini London.
  Liverpool ilitangulia kwa mabao ya washambuliaji wake tegemeo wa Kiafrika, Msenegal Sadio Mané dakika ya tisa na Mmisri, Mohamed Salah dakika ya 26, kabla ya Chelsea kusawazisha kupitia kwa Mateo Kovacic dakika ya 42 na Christian Pulisic dakika ya 45.
  Chelsea inafikisha pointi 43, ingawa inabaki nafasi ya pili ikizidiwa pointi 10 na mabingwa watetezi, Manchester City baada ya wote kucheza mechi 21, wakati Liverpool inafikisha pointi 42 katika mchezo wa 20 nafasi ya tatu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: CHELSEA YAAMBULIA SARE KWA LIVERPOOL, 2-2 DARAJANI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top